Waliofariki shambulio Baghdad wafika 250
Wizara ya afya nchini Iraq inasema kuwa idadi ya watu ambao sasa
wanajulikana kuuawa kwenye shambulizi la kujitolea mhanga siku ya Jumapili
mjini Baghdad imeongezeka hadi watu 250.
Shambulizi hilo ambalo kundi la Islamic State lilidai kutekeleza, ndilo baya zaidi
kuwai kutokea mjini Baghdad tangu Marekani iongoze uvamizi nchini Iraq
mwaka 2003.
Ripoti ya Uingereza kuhusu uvamizi huo inatarajiwa kuchapishwa hii leo.
Mwenyekiti wake anasema ana matumaini kuwa ripoti hiyo itahakikisha kuwa
kuingilia kati kwa njia ya kijeshi kiwango kama hicho, hakuwezi kutokea siku za
usoni bila ya kufanyika udadisi kwa njia ya uangalifu mkubwa.
2. Mfalme wa Saudia kukabili hatari ya mashambulio
Mfalme Salman wa Saudi Arabia ameahidi kuchukua hatua kufuatia misururu ya
mashambulizi ya kujitolea mhanga.
Akiyataja makundi yenye itikadi kali, Salman alisema kuwa atawakabili vikali
wale wanaojaribu kuvuruga akili za vijana wake. Alikuwa akiongea siku moja
baada ya maafisa wanne wa usalama kuuawa na bomu karibu na eneo takatifu
mjini Medina.
Pia kulikuwa na mashambulizi mengine mawili maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Inaaminika kuwa Islamic State ndio walihusika kwenye mashambulizi hayo
ambayo yamelaaniwa na madhehebu ya Sunni na Shia.
3. Mwanabalozi aliyetekwa Nigeria aachiliwa huru
Naibu balozi wa Sierra Leone nchini Nigeria ambaye alitekwa nyara Ijumaa
iliyopita ameachiliwa huru. Meja Jenerali alitekwa nyara katika mkoa ulio
kaskazini wa Kaduna, akiwa na dereva wake raia wa Nigeria.
Taarifa kidogo imetolewa na maafisa kutoka nchi zote lakini anaripotiwa kuwa
katika afya nzuri. Afisa kutoka nchini Sierra Leone anasema kuwa hakuna fidia
ililipwa
Visa vya utekaji nyara ni tatizo kusini mwa Nigeria lakini sasa vinasambaa
kwenda kaskazini mwa nchi.
4. Amnesty yasema maelfu wameathirika kiakili Sudan Kusini
Shirika la Amnesty International linasema kuwa maelfu ya watu nchini Sudan
Kusini wana matatizo ya akili yanayotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe
na wengi hawana matumaini ya kupata matibabu.
Amnesty inasema kuwa watu wamelazimishwa kula nyama ya binadamu wakati
wa mzozo huo ambao ulianza mwishoni mwa mwaka 2013.
Inasema kuwa kuna uhaba mkubwa wa huduma za kiafya kote nchini humom
huku mara nyingi watu walio na matatizo ya akili hufungiwa gerezani.
5. Obama ampigia kampeni Clinton
Rais wa marekani Barack Obama ameonekana kwa mara ya kwanza kwenye
kampeni ya mgombea urais wa Democtratic Hillary Clinton. Mapema shirika la
ujasusi nchini marekani FBI liolisema kuwa hakuna mashtaka dhidi ya Bi
Clinton kuhusu kutumia E-mail yake ya kibinafsi kutuma na kupokea ujumbe wa
siri wakati akiwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni. Hata hivyo mpinzani
wake wa Republican amesema kuwa Bi Clinton kutofunguliwa mashtaka
inaonyesha kuwa uchaguzi tayari umevurugwa.
"Habari hii ni kwa mujibu wa BBC"
No comments