NASHUKURU MUNGU KWA KUUTUA MZIGO SALAMA HUKU NIKIIACHA NCHI IKIWA SALAMA TULII KABISA - DKT. JAKAYA KIKWETE


Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya
Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha
Mapiduzi katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo
mstaafu wa CCM , iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani .
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na Mke
wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ,mama Salma Kikwete, katika
hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa
CCM ,iliyofanyika wilayani Bagamoyo ,wengine ni wabunge wa mkoa
huo wakimsalimia Mwenyekiti huyo mstaafu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM ).
wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi wakimsikiliza
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya
Kikwete katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo
mstaafu wa CCM ,iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo .
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya
Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbili wa
mkoa wa Pwani . 



PWANI.
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt .Jakaya
Kikwete amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama
huku akiicha nchi ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea
wilayani hapo ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza
nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia flaha kurudi tena
Bagamoyo akiwa salama .

Amesema wakati akielekea kutanga nia ya kugombea urais alikuwa
na mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika
na Ridhiwani anachapa kwenye Komputa .

Dkt.Kikwete ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo katika hafla ya
kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi ,
ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani .

Alisema . anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoazia na
kwamba amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na
imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi. Akikumbuka mchakato wa
mwakajana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini
mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .

" Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na
wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumayi " amesema
Dkt. Kikwete .Aidha amesema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo
kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake
hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani .

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa
ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote
bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya
kunyoshewa vidole hususani pale alipojalibu kupeleka maendeleo
Wilayani Bagamoyo konakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa
hawana haki .

Aidha Dkt. Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi
wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita ,
Sengerema ,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi
kufikia wabunge kulumbana.

Amesema hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa
Bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea
maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga mkono .

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo
wamejitokeza Kwa wingi kumkaribisha nyumbani Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama hicho Dkt .Jakaya Kikwete katika sherehe
zilizofanyika wilayani Bagamoyo . Wanachama hao ambao walitoka
katika wilaya zote za Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mwenyekiti
wa Chama hicho mkoa Masikuzi. pamoja na Katibu Joyce Masunga
walimuaga na kumkaribisha Kwa nyimbo mbalimbali.




No comments