Wizara zote zatakiwa kuhamia Dodoma

Agizo la Rais Dk John Magufuli la kuzitaka wizara zote kuhamia Dodoma
limeanza kutekelezwa ambapo ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za
mitaa (TAMISEMI) imeandaa mipango maalum wa kuboresha mji wa Dodoma
ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu ya uhakika ya barabara nishati ya
umeme na maji ili kuweza kumudu ongezeko la watu wanaotarajiwa kuhamia
mkoani humo.

Akizungumzia mipango hiyo naibu waziri ofisi ya rais TAMISEMI Mhe Suleiman
Jafo amesema miongoni mwa mambo yatakayoanza kutekelezwa kwa haraka ni
pamoja na kuboresha miundombinu na kutenga maeneo tofauti ya ujenzi wa
ofisi za serikali ili kuepuka msongamano huku akiziagiza halmashauri zilizoko
pembezoni mwa mji wa Dodoma kutumia fursa ya makao makuu kujenga miji
ya kisasa ambayo itakuwa chanzo cha mapato ya uhakika kwa halmashauri
husika.

Katika hatua nyingine naibu waziri Jafo ametembelea wilaya ya Chemba ili
kuzungumza na watumishi na kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ambapo amebaini ubadhilifu mkubwa katika utekelezaji wa miradi mitano ya
maji uliofanywa na maofisa kutoka wilaya mama ya Kondoa na kuagiza
wahusika wake ambao tayari aliwasimamisha kazi kukamatwa mara moja na
kufikishwa mahakamani.

Awali akitoa taarifa ya ugonjwa wa ajabu uliosababisha vifo vya watu 13
ambao chanzo chake ilikuwa ni wilaya ya Chemba mkuu wa wilaya hiyo Husen
Mashimba amesema uchunguzi uliofanywa na mkemia mkuu wa serikali
umebaini kuwa ni ugonjwa wa sumukuvu ambao chanzo chake ni fangasi
anayeshabulia mazao yaliyohifadhiwa vibaya baada ya kuvunwa na mpaka hivi
sasa wapo wagonjwa watatu wakiendelea kutibiwa.
y











No comments