Iceland yapokewa kifalme
Maelfu ya raia wa Iceland wamekusanyika katikati ya mji mkuu wa Reykjavik
kukaribisha msafara wa timu yao ya taifa kwa mafanikio iliyopata kwenye
michuano ya Kombe la mataifa Bingwa barani ulaya mwaka huu 2016.
Wachezaji walipita katikati ya mji wakiwa ndani ya basi kubwa la wazi
wakisindikizwa na ngoma hadi katika mlima wa Arnarholl ambapo mashabiki
waliwasalimia kwa shangwa na makofi .
Iceland ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza mashindano makubwa ya
Kombe la mataifa barani Ulaya ilifikia ukingoni mwa mashindano mwaka huu
baada ya kupata kichapo kutoka kwa Ufaransa kwa magoli 5 – 2.
Hata hivyo kabla ya kuondolewa ilionyesha maajabu pale ilipoiondoa England
kwenye hatua ya kumi na sita bora.

No comments