Mke wa Trump adaiwa kuiba hotuba ya Michelle Obama
Sherehe ya ufunguzi wa kongamano kuu la wajumbe wa chama cha Republican
nchini Marekani imegubikwa na utata baada ya hotuba iliyotolewa na mke wa
Donald Trump, Melania kuwa na maandishi yaliyotolewa kutoka kwenye hotuba
ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle, aliyoitoa miaka minane iliyopita.
Mke huyo wa Trump, ambaye ni mzaliwa wa Slovenia, amesema alipata usaidizi
mdogo sana wakati wa kuandika hotuba hiyo, ambayo imesisitiza sana maadili
ya kifamilia na kujumuishwa kwa watu wa matabaka yote.
Sehemu moja ya hotuba ya Bi Trump alisema: "Wazazi wangu walinifunza
umuhimu wa kutia bidii kutafuta unachotaka maishani; kwamba neno lako ndilo
linaweka uhusiano na unafaa kutenda unachosema na kutimiza ahadi; kwamba
lazima uwaheshimu watu.”
Hotuba ya Bi Obama mwaka 2008 ilisema: "Mimi na Barack tulilelewa na
maadili karibu sawa, kwamba unatia bidii kutafuta unachotaka maishani;
kwamba neno lako linaweka uhusiano na kwamba unafaa kutenda unachosema
utatenda; kwamba lazima uwaheshimu watu, hata kama huwafahamu, na hata
kama haukubaliani nao.”
Maafisa wa kampeni wa Bw Trump hawajajibu madai hayo.
Wengi wa waliohutubu katika kongamano hilo linaloendelea mjini Cleveland,
Ohio, wameangazia sana kutilia shaka uwezo wa mgombea wa chama cha
Democratic Hillary Clinton kuwa rais.
Meeya wa zamani wa New York Rudy Giuliani amewauliza wajumbe:
“Nani anaweza kumwamini Bi Clinton amlinde?”
Awali, wajumbe wanaompinga Bw Trump waliandamana na kulalamika baada
yao kuzuiwa kuwasilisha pingamizi zao.
Chama cha Republican kinatarajiwa kumtangaza Trump kuwa mgombea wake
wa Urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.B

No comments