Deni la biskuti lasababisha mauaji

Mtu mmoja na mkewe kutoka jamii ya Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini
India wameuawa, mmoja akiwa amekatwa kichwa na mwingine kunyongwa kwa
kushindwa kulipa deni la Rupee kumi na tano ambalo ni karibu senti ishirini na
mbili tu, BBC imeripoti.

Polisi kaskazini mwa taifa hilo wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana
mfanyi biashara anayetokea jamii ya hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao kwa
kushindwa kulipa deni la biskuti walizokuwa wamewachukulia watoto wao.
Mfanyabiashara huyo amekamatwa.

Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii
ya Daliti waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye
daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo 'caste'
ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika lindi
la umaskini .

Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la
Gujarat vimeongezeka mnamo siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la
maandamano kutoka watu wa jamii hiyo.

BBC











No comments