Waziri Mkuu Majaliwa adai atahamia Dodoma mwezi wa tisa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametii lile agizo la viongozi wote kuhamia
mjini Dodoma huku akisema yeye atakuwa wa kwanza kuhamia huko.
Ameyasema hayo Jumatatu hii katika maadhimisho ya kuwakumbukua
mashujaa waliolipigania taifa yaliyofanyika mjini humo. Amewaambia wakazi
wa Dodoma kuwa mnamo mwezi wa tisa atakuwa tayari ameshahamia
huko.
“Nimemuita waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na katibu mkuu,
nimewaambia wakamilishe nyumba yangu nahamia mwezi wa tisa haraka
sana pale juu mara moja,” alisema.
“Kwahiyo mimi nikitangulia mwezi wa tisa mawaziri wote wanifuate. Moja
tuhakikishe Dodoma ni kisiwa cha amani na pili watu wanakuja na
tunaamini mamaziri, mabalozi wanaotoka nje watakuja Dodoma, tunahitaji
huduma mbalimbali Dodoma, jipangeni sasa kuwekeza serikali hii ilivyosema
tunatoa fursa hizi ndio fursa.
Ongezeni hoteli za kitalii, ongezeni nyumba za
kulala wageni, jengeni mahoteli makubwa, andaeni mazingira ya nyie kupata
tija kufuatia ujio wa mawaziri mbalimbali na wageni kutoka nchi mbalimbali,
huo ndo wito wangu,” alisisitiza.
Pia aliwashukuru wote walioudhuria maadhimisho hayo na kumshukuru Rais
John Pombe Magufuli kwa kumpa nafasi ya kuongea na wananchi wa
Dodoma na Watanzania kwa ujumla.
No comments