Agizo la Makonda lapingwa kila kona

Wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa nchini, kupitia mitandao ya kijamii
wamepinga agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda la
kuliagiza Jeshi la Polisi mkoani Dar es salaam kuwasaka wananchi ambao
hawana kazi maalum.

Kulingana na taarifa iliyopatikana kwenye mitandao ya kijamii jana, Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, alitoa taarifa kuwa wakati wowote jeshi
la Polisi mkoani humo litaanza msako wa nyumba kwa nyumba kuwasaka
wasiokuwa na Kazi maalum za kufanya.

Agizo hilo linaenda sambamba na kutaka ushirikiano wa viongozi wa serikali za
mitaa, viongozi ambao hawatatoa ushirikiano watakamatwa.
Mmoja wa wadau aliyetoa maoni yake ni aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu
chama cha Wananchi CUF(Bara) Julius Mtatiro ambapo amesema agizo hilo
halikidhi matakwa ya kisheria pia ni kinyume na maadili.
Aidha, Mtatiro ametahadharisha kuwa agizo hilo linaweza kuzua vurugu,
machafuko mitaani.

Naye Meya Wa Jiji la Dar es salaam mstahiki Issaya Mwita Charles amesema
agizo hilo sio kipaumbele cha mkoa wa Dar es salaam.
Mstahiki Meya amesema zoezi hilo ni batili Na haliwezi kutekelezeka kwenye
Halmashauri za Jiji la Dar esSalaam.

Mwita ametoa sababu nne za kupinga agizo hilo;
Amesema Sheria ya makosa ya Jinai inaelezea utaratibu wa kukaguliwa
nyumbani kama 'search warrant' ambayo inatolewa Na Mahakama au polisi, Na
ambayo Inaelezea wanatafuta nini.

Pia amesema Sheria hiyo inamtaka mwananchi kuwakagua maafisa wa
Mahakama Na Polisi watakaofika Nyumbani kwake ili wasiweze kumpandikizia
ushashidi wa uongo.

Kadhalika amesema kibali cha wananchi kukaguliwa majumbani hakiwezi
kutolewa Na Viongozi wa kisiasa.
Amesema hakuna sheria Tanzania zinazoruhusu wananchi kuwekwa ndani kwa
sababu zisizo na msingi hivyo amewataka wananchi kupuuza agizo hilo kwa
kuwa ni kinyume na matakwa ya kisheria.

Tangu kutolewa kwa agizo hilo, kumekuwa na mijadala mirefu kwenye mitandao
ya kijamii wengi wakitoa maoni yanayopinga agizo hilo la Mkuu wa Mkoa.


No comments