NAGU:Wananchi shirikianeni kutunza Miradi ya maendeleo
Ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inadumu,Wananchi wa kata ya Endagaw Wilayani Hanang’ mkoani Manyara wametakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kuitunza ili iweze kuwasaidia sasa na hata
vizazi vijavyo.
Mbunge wa Jimbo la Hanang’ Dkt. Mary Nagu ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kijiji cha moram Kata ya Endagaw ambapo amesema kuwa ni vema wananchi wakatambua kuwa miradi hiyo imetumia gharama kubwa na ni kwa manufaa yao .
Amesema kwamba ujenzi wa soko la mazao la kimataifa lililopo
katika kata hiyo umekamika hivyo ni lazima waweke
mfumo madhubuti wa soko hilo ili kuweza kuleta manufaa kwa
wananchi wa Wilaya hiyo.
Ndugu zangu ujenzi wa soko letu la Kimataifa umekamilika na soko ni mfumo, ni lazima tuweke mfumo madhubuti wa kuendesha soko lile ili liweze kutusaidia, bila kufanya hivyo tutajikuta tunashindwa kunufaisha wana Hanang’ na badala yake watanufaika watu wa kutoka nje ya hapa’’ Alieleza Dkt. Nagu.
Alisema kuwa soko hilo litawaweka pamoja wananchi waKata ya Endagaw na Hanang’ kwa ujumla ambapo wao ndio wataamua kuuza mazao yao kwa bei ya kimataifakwa kuwa ni soko la kimataifa, si kama ilivyo sasa ya kupangiwa bei na wanunuzi.
Aidha alisema kwamba ni lazima viongozi wawekemfumo madhubuti wa kuwaletea vijana maendeleo kwa kuwapatia ajira katika soko hilo na hiyo itasaidia kufanyika shughuli za kiuchumi katika wilaya yao na uchumi wao utaimarika maradufu.
Kwa upande wa mradi wa umwagiliaji, Mhe: Nagu alisema kuwa Nchi haina uhakika wa mvua za kutosha hivyo ni miradi ya umwagiliaji tu ndio itawahakikishia chakula cha kutosha na mazao ya biashashara.
‘Ninaomba muwe na mpangilio mzuri ili manufaa yawe makubwa na muangalie tija ya maeneo
ya umwagiliaji kwa kupangilia mazao ya kulima katika maeneohayo’’ Alisisitiza Nagu.
Naye Mtendaji wa Kata ya Endagaw Bw. Yusuph Jackson alisema kuwa ujenzi wa soko la mazao la kisasa ambalo limekamilika na hivyo wanaomba kufunguliwa mapema ili wananchi waweze kuuza mazao yao na kufaidika na ujenzi wa soko hilo katika kata yao.

No comments