SUMATRA YAIFUNGIA KAMPUNI YA MABASI YA CITY BOY AMBAYO MABASI YAKE MAWILI YALISABABISHA AJALI JANA


Siku moja baada ya kutokea ajali ya mabasi mawili na kusababisa vifo vya watu 30 na majeruhi kadhaa, Kampuni ya mabasi ya City Boy
imefungiwa kufanya biashara hiyo kwa muda usiojulikana .

Ajali hiyo ilitokea eneo la Maweni , Manyoni , mkoani Singida baada ya
mabasi ya kampuni hiyo , moja likitokea Dar es Salaam na lingine
likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam kugongana

Msemaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra), David Mziray amesema leo kuwa kampuni hiyo ina miliki
mabasi 12 na yote yamefungiwa kufanya safari yoyote kuanzia leo .

“ Mabasi hayo yamefungiwa kuanzia leo kwa muda usiojulikana,
ukaguzi wa mabasi yao utaanza kufanyika kupitia jeshi la polisi,”
amesema Mziray.

No comments