SEMBOSI: EPUKENI MAONYESHO YA MAZOWEA.

Maandalizi ya maonyesho 23 ya Kilimo na sherehe za nanenane mwaka 2016 yanaenendelea huku yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo Kilimo Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya maeneleo :Vijana shiriki kikamilifu 'Hapa kazi tu'

Hayo yamesemwa na Katibu wa TASO Kanda ya Kaskazini Jeremia Solomon Sembosi huku akiwatakawashiriki kuondokana na maonyesho ya mazowea,bali wahakikishe teknolojia zinazoletwa kwenye maonyesho zifuatiliwe,wapanue wigo mpana katika jamii kwa ujumla.

Pia amewataka washiriki kuweka rekodi zao vizuri ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye jamii na watu waepukane na mitizamo hasi ya kutokuwa na malengo ya kujifunza kwenye maonyesho badala yake wajipange vizuri kuwa na taarifa nzuri zinazouzika kwa wananchi wanaokuja kutembelea mabanda yao ili wapate kuelewa kwa ufasaha.

Pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote wawalete wananchi ambao watakuja kujifunza nakupata elimu ambayo itawasaidia baada ya maonyesho kumalizika,ili baadae wakafanye vizuri ili nawao wakatoe elimu kwa wenzao kwenye maeneo ambayo wanatokea.

Aidha Sembosi amesema kuwa baada ya maonyesho kumalizika washiriki wote watatakiwa kutoa ripoti namrejesho wakile ambacho wananchi wameelewa kutokana na maonyesho hayo pamoja na teknolojia walizozileta katika maonyesho wananchi wamezielewaje na wanazitendeaje kazi.

Maonyesho hayo ya Kilimo na sherehe za nanenane mwaka 2016 ya natazamiwa kuwa na washiriki zaidi ya mia mbili na watazamaji wa maonyesho zaidi ya laki mbili,ambapo wanatazamia kuwa na mgeni rasmi mwenye hadhi ya kitaifa ambapo atafahamika hapo baadae kwa mujibu wa Katibu huyo.



No comments