Mtitu awashukia viongozi TAFF
DAIREKTA mwenye jina kubwa nchini, William Mtitu amefunguka kuwa kitu
kinachoiangusha tasnia ya filamu Bongo ni uongozi wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF), ambao umeshindwa kuwasimamia wasanii wake vizuri pamoja
na kutengeneza mazingira mazuri ya kuwafanya wadau mbalimbali kuvutiwa na
tasnia hiyo hata kuwekeza.
Akihojiwa na GPL, Mtitu aliongeza kuwa ili tasnia ya filamu iweze kusimama na
kusonga mbele au angalau tu kurudi mahala ilipokuwa siku za nyuma ni lazima
uongozi wa TAFF uwe thabiti ikiwezekana yafanyike mabadiliko makubwa katika
uongozi huo na wapatikane viongozi wazuri wa kuwasimamia wasanii katika
ukuzaji wa tasnia ya filamu.
“Unapoona kundi lenye viongozi linashindwa ni dhahiri kuwa viongozi wake si
thabiti. Ndivyo ilivyo kwenye filamu, hii sintofahamu inayoendelea iliyoshusha
tasnia yetu ni ukweli kuwa huwezi kuwalaumu tu wasanii, viongozi wa TAFF
wanahusika kwa namna moja au nyingine,” alisema Mtitu.N

No comments