RAIS MAGUFULI AMTEUA PROFESA KABUDI KUWA MWENYEKITI MPYA WA BENKI YA TIB
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa
kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria
(Interpretation of Laws Act) Sura 1, leo tarehe 5 Julai,
2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki
ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa .
Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo
chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya
umma (Public Corporations Act) Sura 257, Mhe. Rais
amemteua Prof. Palamagamba J. A. M.
Kabudi (pichani)kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya
Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka
mitatu.
Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Philip Isdor Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa
mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri
za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, ametengua
uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
Aidha, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya
kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma
(Public Corporations Act, Sura 257) Mhe. Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua
wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha
miaka mitatu:
1. Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
2. Dkt. Razack B. Lokina.
3. Bi. Rose Aiko
4. Prof. Joseph Bwechweshaija
5. Bw. Said Seif Mzee
6. Dkt. Arnold M. Kihaule
7. Bw. Maduka Paul Kessy
8. Bw. Charles Singili
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi
unaanza tarehe leo 5 Julai, 2016.
*Gerson Msigwa.*
No comments