DC awaweka ndani maafisa wa afya Kahama

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu amewatia mbaroni maofisa afya wa
halmashauri ya mji wa Kahama kwa tuhuma za kuacha uchafu katika barabara
kuu ya mji wa Kahama ya kwenda katika nchini za jirani za Rwanda na Burundi
zikitoa harufu mbaya.

Maofisa walioswekwa ndani ni Johanes Mwebesya na mtendaji wa kata ya
Nyasumbi Enocent Kapeli wanaotuhumiwa kuacha wananchi wakitupa taka
katika eneo lisilostahili eneo lililopo mwanzo mwa barabara kuu ya kuingia
katika mji wa Kahama eneo la Phatom.

Awali mkuu huyo wa wilaya alipita eneo la phatom akielekea halmashauri ya
Ushetu kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kawaida ndipo aliona rundo la uchafu
katika barabara hiyo kuu ya kuingia Kahama Mjini, jambo ambalo alieleza
linaleta sura mbaya kwa mji wa Kahama.

Alitoa maagizo kabla ya kuondoka kwenda Halmashauri ya Ushetu mbele ya
Mkurungezi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson Msumba pamoja na
Mtendaji wa kata hiyo na Ofisa Afya wa kata hiyo kuwa akirudi kutoka Ushetu
akute uchafu huo umeondolewa hapo haraka jambo ambalo halikutekelezeka.




No comments