Dkt. Mkoko: Wanablog Zingatieni Habari za Uchaguzi Zichapishwe kwa Ukweli na Uthibitisho.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Bloga
nchini Tanzania wametakiwa kuhakikisha vinachapisha taarifa za kweli,
sahihi na zinazoweza kuthibitishwa, sambamba na kuzingatia maadili ya
taaluma ya uandishi wa habari, ili kulinda amani na mshikamano wa
kitaifa.
Kauli
hiyo imetolewa na Dkt. Egbert Mkoko, Mhadhiri katika Shule Kuu ya
Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), wakati akitoa mada ya
Mwongozo wa Habari katika Uandishi wa Habari za Uchaguzi kwenye mafunzo
ya wanabloga wa Tanzania (TBN) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025,
yaliyofanyika katika makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) jijini Dar es Salaam.
Amesema
ni wajibu wa wanahabari na wanabloga kuhakikisha kila taarifa
inayochapishwa inatokana na vyanzo vinavyoaminika, kuepuka upendeleo wa
kisiasa na kuchochea maudhui yenye kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Dkt.
Mkoko amesisitiza kuwa katika kipindi cha kampeni na uchaguzi, taarifa
zisizo sahihi zinaweza kusababisha taharuki, hivyo umakini na weledi
unahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Miongoni
mwa mada zilizotolewa ni mwongozo wa habari katika uandishi wa habari
za uchaguzi, ambapo washiriki walipata elimu kuhusu umuhimu wa uandishi
wa habari unaozingatia ukweli, usawa na uadilifu, pamoja na athari za
taarifa za upotoshaji katika kipindi cha uchaguzi.
Katika
tukio hilo, washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali, kushiriki
majadiliano na kubadilishana uzoefu, sambamba na kupewa mwongozo wa
namna ya kutumia mitandao ya kijamii kwa njia salama na yenye tija.
Aidha,
amepongeza TCRA kwa wapata mafunzo Mabloga wa Tanzania Bloggers Network
(TBN) ambayo yataleta mabadiliko chanya katika namna taarifa za
uchaguzi zitakavyoripotiwa, na hivyo kusaidia wananchi kupata hab
No comments