Bodi MSD Yawavua Ukurugenzi Waliosimamishwa na Waziri
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(Mb.
BODI ya Wadhamini ya Bohari ya Madawa nchini (MSD) imewavua
ukurugenzi wakurugenzi wawili waliosimamishwa kazi hivi karibuni na
kumfukuza kazi mmoja baada ya kukutwa na makosa kwenye uchunguzi
uliofanywa juu ya tuhuma mbalimbali dhidi yao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya
MSD, Laurean Bwanakunu jijini Dar es Salaam inasema waliovuliwa
ukurugenzi ni Bw. Joseph Tesha na Misanga Muja aliyekuwa Mkurugenzi
wa Ugavi wa MSD.
Taarifa inasema Bw. Cosmas Mwaifwani ambaye alikuwa Mkurugenzi wa
Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wajeja, ambaye pia alisimamishwa
kupisha uchunguzi amepatikana na kosa hivyo amefukuzwa kazi kuanzia
Julai 8,2016 kwa kufuata sheria na kanuni za SMD.
Taarifa ya Bwanakunu inasema Bw. Heri Mchunga ambaye ni niongoni
mwa maofisa waliosimamishwa ameonekana hana hatia hivyo
amerudishwa kazini na kuhamishiwa Kurugenzi ya Ugavi kushika nafasi ya
Mkurugenzi.

No comments