Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Asimamishwa Kazi Kwa Kosa la Kulipa Malipo Hewa


UKatibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest
Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Frank Charles
Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani kulipa posho ya
chakula kwa watu ambao si askari.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata,
Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki anasimamishwa kazi kwa kufanya
malipo ya kiasi cha sh. 305,820,000 kama posho ya chakula kwa watu
ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi
2015/2016.

Meja Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na
Taratibu za Kijeshi anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration
allowance’ ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.
Meja Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo
tangu leo tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma
zinazomkabili.

Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na
Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi
imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili kufanikisha malipo hayo
hewa

No comments