Wanafunzi hewa kuondolewa vyuoni
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako, amesema operesheni ya uhakiki wa wanafunzi hewa wanaopatiwa
mikopo imeanza kuonesha mafanikio, kwani wanafunzi hewa wameanza
kubainika.
Akizungumza baada ya kufungua Maonesho ya 11 ya Elimu ya Juu, Sayansi na
Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) jana, alisema
uchunguzi wa awali umebaini wanafunzi hewa 139 katika vyuo vitano
vilivyofanyiwa uhakiki.
“Tunaendelea kuhakiki na tayari tumehakiki vyuo vitano ambapo wanafunzi
hewa 139 walibainika kati yao wamo marehemu, walioacha shule,
waliosimamishwa shule na waliohamishwa,” alisema bila kuvitaja vyuo hivyo
kwa maelezo kuwa, taarifa haijawa kamili.
Aidha, alisema katika jitihada za kuboresha elimu inayotolewa nchini wizara
hiyo inafanya mapitio ya Sheria ya Vyuo Vikuu ili itoe fursa kuchukulia hatua
vyuo vya kitapeli. Alisema kupitia sheria hiyo, serikali itaanzisha mfumo wa
kuratibu na kudhibiti uanzishwaji wa vyuo kwa lengo la kuwabana
wanaoanzisha vyuo kwa lengo la utapeli.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli aliwasimamisha kazi watendaji wakuu wa
Kamisheni ya Tume vya Vyuo Vikuu (TCU) baada ya kubainika kamisheni hiyo
inadahili wanafunzi wasio na sifa, wakiwemo wenye ufaulu wa daraja la nne,
kujiunga na vyuo vikuu na kuwapatia mikopo.
Serikali pia ilibaini uwepo wa wanafunzi hewa wanaotafuna mikopo ya elimu ya
juu, jambo lililosababisha Profesa Ndalichako kutangaza vita dhidi yao na
kuanza operesheni ya uhakiki katika vyuo vyote vikuu nchini.
Aliungwa mkono na Rais John Magufuli aliyetangaza kuwa serikali yake
imejipanga kumaliza makosa yote yaliyojitokeza huko nyuma, ikiwemo tatizo la
watumishi na wanafunzi hewa lililoibuka hivi karibuni.
Profesa Ndalichako alianza kuchukua hatua kwa kusimamisha kazi viongozi
wanne waandamizi kwa tuhuma za kudahili wanafunzi wasio na sifa.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya TCU, Awadh Mawenya naye alisimamishwa kazi
kwa kosa la kushindwa kuwachukulia hatua watumishi waliodahili wanafunzi
hao wasio na sifa.
Profesa Ndalichako alichukua hatua hizo baada ya TCU kudahili wanafunzi 489
waliopata daraja la 4.32 katika mitihani yao ya kidato cha nne lakini walijiunga
na chuo kikuu na kupatiwa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 784
H
V
No comments