Lowassa awataka vijana wajipange kuelekea 2020
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA
ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa amelitaka baraza la
vijana la CHADEMA Taifa kutokukubali kugawanywa katika misingi ya kisiasa na
badala yake wajikite katika kukiimarisha chama hicho katika ngazi ya chini hasa
vijijini.
Waziri huyo mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA
Taifa ametoa rai hiyo kwa vijana wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa
kamati tendaji ya BAVICHA Taifa na ambapo amehimiza umoja ndani ya baraza
hilo na kuwataka kuelekeza nguvu zao mwaka 2020 huku pia akiendelea
kusikitishwa na kauli tata za katazo la mikutano ya kisiasa.
Lowassa amesema kuwa amesikitishwa na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya
vyama vya siasa wakati ikikiruhusu chama cha Mapinduzi(CCM) kufanya
mikutano.
Aidha, Lowassa amedai kushangazwa na kauli ya Kamanda wa Polisi wa mkoa
wa Dodoma kuhusu kuiruhusu CCM kufanya mkutano wa hadhara kwenye
uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, mkutano ambao utatumika
kumtambulisha Dk Rais John Magufuli kama mwenyekiti mpya wa CCM.
John Mrema na Bw. Patrobas Katambi ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo
pamoja na masuala mengine wamewataka vijana kuwa mstari wa mbele
kuhakikisha demokrasia inapatikana huku pia adhima yao ya kuelekea mjini
dodoma wakisema iko pale pale
Kikao hicho cha kamati kuu tendaji ya BAVICHA Taifa kilihudhuliwa na wajumbe
kutoka mikoa yote Tanzania ambapo pia kinaratajia kutoka na azimio la njia
No comments