UKAWA wasusia hafla IKULU
Vyama vya upinzani vimesusia hafla iliyoandaliwa Ikulu kwa ajili ya Rais Paul
Kagame wa Rwanda.
Rais John Magufuli alikuwa ameandaa dhifa ya kitaifa kwa ajili ya mgeni huyo
ambaye aliwasili nchini juzi kwa ziara ya siku mbili, iliyohusisha kufungua
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuzindua maonyesho hayo, Rais Kagame aliandaliwa hafla hiyo
ambayo ingeweza kumkutanisha na viongozi wengine wa kisiasa na
wafanyabiashara, lakini hali ikawa tofauti baada ya viongozi wa vyama vya
upinzani vinavyounda Ukawa kutoshudhuria.
“Kuna mgogoro huo wa kuzuia mikutano ya hadhara, lakini hawajali. Suala la
Zanzibar, watu wanakufa lakini hawajali, bungeni kuna mpasuko kwa muda
wote lakini hawajali,” amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mbunge wa Hai
akizungumzia uamuzi wao wa kugoma.
*Mwananchi*
No comments