Rais Magufuli Amteua Deogratius Ndejembi Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John
Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa
Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.
Uhamisho wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi,
umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally
Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi,
kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.
Bw. Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa
viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar
es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Julai, 2016

No comments