Ikulu yakanusha uvumi kuhusu Jerry Murro

Kufuatia kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amemuidhinisha Gerson
Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, huku taarifa hiyo ikidai kuwa
Rais pia amemteua aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Murro kuwa
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, taarifa hizo sio za kweli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na
kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa ni kwamba Rais
hajafanya uteuzi huo.

"Kuna taarifa zimesambazwa zikisema kuwa Rais Magufuli amemthibitisha
Gerson Msigwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu huku msaidizi wake
akiwa ni aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Murro, taarifa hizo sio za
kweli na wananchi wazipuuze," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imesema maamuzi yoyote ya uteuzi wa rais yatatangazwa na
kuwekwa kwenye tovuti ya Ikulu kama ilivyo kawaida.







No comments