Askari Polisi Auawa Kwa Kupigwa Risasi akiongoza magari usiku Kijitonyama Dar es Salaam
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi
Oysterbay ameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa risasi akiwa kazini
eneo la Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema
tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo
hakijafahamika.
“Tukipata chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa
tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema Fuime.

No comments