Ajali ya basi yaua watano Korogwe


Watu watano waliokuwa wanasafiri kwa basi la kampuni ya Mbazi kutoka Dar
es Salaam kwenda Arusha wamekufa na wengine 28 kujeruhiwa baada ya basi
lao kupinduka katika Kijiji cha Chekelei, wilayani Korogwe.

Watatu walikufa katika eneo la tukio, huku wengine walikufa baada ya
kufikishwa hospitalini.

Ajali huyo imethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, David
Mnyambugha, akisema ilitokea Julai 18, mwaka huu majira ya saa 11.30 jioni.
“Juzi jioni basi hilo namba T 587 APN aina ya Scania lilikuwa likitoka Dar es
Salaam kwenda Arusha lilipofika eneo la Chekelei ghafla mwendesha baiskeli
alivuka barabara, hivyo dereva wa basi ambaye sijapata jina lake alijitahidi
kumkwepa, lakini alishindwa na ndipo gari likapinduka,” alisema na kumtaja
mwendesha baiskeli kuwa ni Ramadhani Mdoe (65), mkazi wa Kijiji cha
Kivilicha.

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo, akiwemo Zuberi Mwindadi alisema mwendo
kasi wa dereva ulichangia kutokea kwa ajali hiyo, kauli iliyoungwa mkono na
majeruhi mwingine, Grace Raymond



No comments