Rais Magufuli amteua Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Prof. Sylvester Michael Mpanduji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Viwanda Vidogo (SIDO).

Taarifa iliyotolewa jana Ikulu Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Sylvester Michael Mpanduji
umeanzia jana tarehe 18 Julai, 2016.

Kabla ya uteuzi huu Prof. Sylvester Michael Mpanduji alikuwa Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Prof. Sylvester Michael Mpanduji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi
Omary Jumanne Bakari ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amemteua Dkt.Winnie Mpanju-Shumbusho kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Hospitali ya Benjamini Mkapa - Dodoma.

Kabla ya Uteuzi huo, Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho alikuwa Mkurugenzi Mkuu
Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) lenye makao yake makuu Mjini
Geneva nchini Uswisi na alimaliza mkataba wake tangu Mwezi Desemba 2015.
Uteuzi wa Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho umeanza jana tarehe 18 Julai, 2016.

Dkt. Winnie Mpanju-Shumbusho anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt.
Donan William Mmbando ambaye ameomba kupumzika kutokana na sababu
binafsi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
18 Julai, 2016u






No comments