MASKINI Babu Seya Hali yake Kiafya Yawa Mbaya..Apelekwa Muhimbili..
Mwanamuziki nguli nchini anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza
Viking 'Babu Seya anadaiwa yu taaban ambapo amekimbizwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.
Mwandishi wetu alimshuhudia Babu Seya akiwa Muhimbili chini ya ulinzi wa
askari magereza watatu na wafungwa wengine watano katika Jengo la
Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) huku akiwa amedhoofu.
Haikuweza kujulikana mara moja ugonjwa uliosababisha Babu Seya
ahamishiwe Muhimbili kwa matibabu kwa sababu Jeshi la Magereza lina
hospitali yake na mwandishi alipoomba kwa mmoja wa askari magereza ili
aweze kumsalimia mwanamuziki huyo, hakupewa ruhusa.
Baadhi ya wananchi waliomshuhudia mwanamuziki huyo akiwa Muhimbili na
kuingizwa katika chumba cha daktari namba 112 walisema, anavyoonekana
ni dhahiri ni mgonjwa kwa sababu hakuwa mchangamfu kama ilivyo
kawaida yake.
“Nguza (Babu Seya) mara nyingi huwa mchangamfu lakini leo amekuwa
mnyonge, mwili umepungua na hata ngozi yake siyo ang’avu, bila shaka
anaumwa sana,” alisema mwananchi mmoja hospitalini hapo.
Hata hivyo, mara baada ya matibabu, Babu Seya aliingizwa katika gari la
magereza na kurudishwa Gereza la Ukonga kuendelea kutumikia kifungo
chake.
Dodosadodosa ya mwandishi hospitalini hapo ili kujua kinachomsumbua
Babu Seya, haikuambulia chochote kwani daktari mmoja alisema ni mwiko
kwao kutaja ugonjwa wa mgonjwa bila ridhaa yake na ni kinyume cha
maadili ya kidaktari.
“Umeniuliza anaumwa nini, kwanza mimi siye niliyemtibu lakini hata kama
ningejua ugonjwa wa Babu Seya, siwezi kukuambia ni unethical (kinyume
cha maadili). Lakini kweli ni mgonjwa na ndiyo maana ameletwa hapa
kutibiwa,” alisema daktari huyo aliyekuwa nje ya jengo moja akizungumza
na mwanamuziki huyo.
Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Dar, Eddy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye Papii Kocha kwa
kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi
Sinza-Mapambano, Dar na kuwafunga kifungo cha maisha jela huku rufaa
ya kesi yao ikiwekwa kiporo kwenye Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu iliyopo jijini Arusha.
No comments