Wema na Idris wadaiwa kuachana
Kulingana na gazeti la burudani la Wikienda, zile mbwembwe zote za penzi la
mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris Sultan, zinadaiwa
kufikia ukingoni na sasa imebaki stori kwani Wema, Idris wamwagana rasmi.
Gazeti hilo linadai kuwa kitendo cha wawili hao ‘kushoo lavu’ kwenye ile Pati ya
Black Tie iliyofanyika juzikati katika Ukumbi wa King Solomoni pale Namanga,
Dar ilikuwa ni geresha tupu kwani walishamwagana kitambo.
Hata hivyo, kama utakumbuka au hukuipata ni kwamba iliwahi kuvujishwa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema na Idris wamemwagana lakini baadaye
'zilivunjwa' picha zikiwaonesha wakiwa wameshikana mikono na mahaba tele ili
'kuua soo'.
Ilidaiwa kwamba, Idris alilazimika kufika kwenye sherehe hiyo kwa sababu
ilishatangazwa kuwa atakuwa ni miongoni mwa ‘ma-hosti’ lakini ukweli ni
kwamba mambo yalishaharibika.
“Unajua watu wengi hawakujua kuwa Wema na Idris walishaachana kitambo na
pale (King Solomoni) walikuwa wanafanya maigizo tu, japokuwa haijulikani
moja kwa moja sababu ya kuachana kwao lakini Wema anadaiwa kuwa tatizo
kwa Idris kutokana na kutokea kwa migogoro ya kila kukicha,” kilieleza chanzo.
Hata hivyo, katika kuonesha kwamba kuna kitu kinaendelea, watoa taarifa
walifuatilia akaunti zote za mastaa hao katika mitandao ya kijamii kuona kama
mbwembwe zao zinaendelea na kubaini kuwa hawako sawa baada ya kusoma
ujumbe wa Wema unaoonesha kumbembeleza Idris huku jamaa huyo akionesha
wazi kuwa hakuna mapenzi bali ni drama tu.
“Having you as a friend, a brother, a lover and of course a shoulder to cry on
every time, i’m at my worst has been the best feeling ever… I wouldn’t want to
lose this feeling over anything…
“I realized without u then i ain’t complete…. You have stood by me in good
times and bad and even when i messed up so bad you would look me in the
eyes and tell me, “Baby, its okay, we gona fix this”…
“Idris you have been one of a kind and losing u is the last thing i want on this
earth… I will love you until forever, until death do us part we will be together…
“I will hold on to you till da last minute because together we will get there…. I
love you with my life…. For I believe you are my true love, my baby and
inshallah! The Man that my kids will call daddy…” alimalizia kuandika Wema
akimlilia Idris.
IDRIS NAYE ALIANDIKA:
“Kumbuka kurekebisha kiatu kila hatua ya maisha unayopiga kisije kuchomoka
ukakanyaga mwiba ukapunguza spidi.”
Wikienda halikuishia hapo kwani lilimsaka Wema anayedaiwa kubwagwa,
alipopigiwa simu hakupokea, akaandikiwa ujumbe mfupi wa sms ambao pia
hakuujibu.
Pia alitumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp lakini pia hakujibu.
Wikienda liligeuza dira yake na kuielekeza kwa Idris ambaye alifunguka bila
kuacha lolote.
Kwa mujibu wa Idris, yeye na Wema walishasahau kuwa waliwahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi kwani kwa sasa kila mtu ana ‘biashara’ zake.
“Mimi nilikwenda kwenye ile pati kwa sababu ya kuwaonea huruma tu kwani
ndiyo kwanza wameanzisha kampuni na mbaya zaidi walikuwa wakiniweka
kwenye matangazo.
"Unadhani watu wangewachukuliaje? Sikutaka kuwaharibia shoo lakini mimi
nilishaachana naye na nina biashara zangu nyingine,” alifunguka Idris.
Idris alienda mbali zaidi na kusema kuwa kwa sasa ana mwanamke mwingine
anayempenda na siku si nyingi mambo yakikaa sawa, atamuanika.
“Mwenzenu nina kifaa kingine soon nitawafahamisha,”
WEMA NA IDRIS
Awali Wema na Idris walificha uhusiano wao lakini baadaye waliamua kujiachia
ambapo mlimbwende huyo alidai kushika ujauzito lakini kwa bahati mbaya
ukachoropoka.

No comments