Mzozo wa ukosefu wa chakula waongezeka Nigeria

Umoja wa mataifa unaeleza kuwa maelfu ya watoto wako
kupoteza maisha kwa ajili ya mzozo wa chakula uanongezeka
katika eneo lilokumbwa na vita la kaskazini mashariki mwa
Nigeria. Dharura hiyo inatokea wakati mbaya kwa Nigeria
ambayo uchumi wake umeathirika kutokana na bei ndogo ya
mafuta na kupungua kwa uzalishaji wa mafuta.

Miaka mingi ya mapigano baina ya vikosi vya usalama na
wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria,
kumevuruga mavuno na kuharibu masoko na kuacha baadhi ya
sehemu kuwa hazipitiki kuwezesha kufikishwa kwa misaada ya
kibinadamu

Matatizo yameongezeka na kuwa mzozo wa chakula ambao
unawaacha watoto katika kanda hiyo kuwa hatarini Zaidi, kwa
mujib wa mratibu wa kikanda wa misaada ya umoja mataifa bw
Toby Lanzer.

Bw. Lanzer anasema, tuna watoto takriban elfu 250 katika eneo
la kaskazini mashariki mwa Nigeria ambao wanautapia mlo
mbaya na tunaweza kupoteza hadi watoto elfu 50 kabla ya
mwisho wa mwaka iwapo hatutaongeza msaada sasa hivi.

Lanzer anasema Nigeria inahitaji dola millioni 164 katika miezi
3 ijayo kusaidia watoto na zaidi ya millioni 4 nyengine katika
nchi ambayo inakabiliwa na ukosefu mbaya wa usalama wa
chakula.

Wiki ilopita, mtandao wa kutoa onyo kwa ajili ya njaa ulieleza
kuwa maeneo ya kaskazini mashariki huwenda tayari
yanakabiliwa na njaa.

Nigeria imekuwa ikikabiliana na harakati za waasi wa Boko
Haram kwa miaka 7 sasa.
Bw Lanzer anasema, hali ya kifedha ya Nigeria ni tete. Na
kutarajia Nigeria kusaidia katika kiwango kinachohitajika
itakuwa ni ombi kubwa sana kutoka jumuiya ya kimataifa.

Uchumi wa Nigeria unategemea mauzo ya nje ya mafuta na
kushuka kwa bei za mafuta duniani pamoja na mashambulizi ya
wanamgambo kwenye mabomba ya mafuta katika eneo la
kuzalisha mafuta la Niger Delta, kumepunguza mapato
yanayoingia kwenye hazina za Nigeria.

Uchumi ulishuka katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,
na mwakilishi wa taifa hilo kwenye shirika la fedha duniani IMF,
aliiambia mtandao wa habari wa Bloomberg News kuwa uchumi
huwenda ukapungua mwaka huu mzima.

Kuchangia matatizo hayo, ni watu waliopoteza makazi wanaoishi
kwenye kambi inaendelea kuongezeka kwa sababu jeshi
limekombowa jamii ambazo zilikuwa chini ya udhibiti wa Boko
Haram.

Mratibu wa idara ya kitaifa ya dharura huko kaskazini
mashariki, Muhammed Kanar anasema wengi wa walowasili
wanakuja kutoka maeneo yasio na chakula au matibabu, na
wananjaa pale wanapowasili.

Kanar alitowa mfano wa kambi ya watu walopoteza makazi
katika mji wa Monguno. Kambi hivi karibuni ilikuwa kutoka
watu elfu 4 hadi elfu 30. Anatarajia idadi hiyo kuongezeka

No comments