Mahafali ya KKKT Chuo Kikuu Muhimbili Yapigwa Marufuku Baada ya Wanafunzi Hao Kumwalika Lowassa Kuwa Mgeni Rasmi

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
umezuia mahafali ya wanafunzi waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT ) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana mchana chuoni hapo
jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa
amealikwa na wanafunzi kama mgeni rasmi.

Mahafali hayo yalizuiwa jana saa 6 mchana ikiwa ni saa mbili kabla ya muda
kuanza
Tangazo lililobandikwa chuoni hapo na kushuhudiwa na wanahabari likiwa
linamnukuu Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Apollinary
Kamuhabwa liliwataka wanafunzi hao kutoweka mikusanyiko ya aina yoyote
chuoni hapo.

Profesa Kamuhabwa kupitia tangazo hilo aliwaonya wanafunzi hao kutojihusisha
na masuala ya siasa wawapo chuoni kama ilivyo kwa watumishi wa umma.
Jitihada za waandishi wa habari kuzungumza na uongozi wa chuo hicho ili
kupata ufafanuzi ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa hawakualika
mkutano na waandishi wa habari.







No comments