UN yahofia uchaguzi DRC kutofanyika
Kiongozi wa tume ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na masuala ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo amenukuliwa akisema nchi hiyo huenda isiweze
kuandaa uchaguzi wa urais hapo Novemba kama ilivyokuwa imepangwa.
Akitoa matamshi hayo asubuhi ya leo, kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mkuu wa tume hiyo Maman Sidikou
ameambia kikao cha waandishi habari mjini Kinshasa kwamba ''ni raia wa
Congo wenyewe ambao wataamua ni lini uchaguzi huo utakapofanyika'.
Maafisa kadhaa katika Umoja wa Mataifa wamekuwa wakionya kwamba
kucheleweshwa kwa uchaguzi huo huenda kukazua upya vurugu na rabsha za
kisiasa nchini humo.
Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya muhula wake
kukamilika.
Hata hivyo, wapinzani wake wasema anachelewesha uchaguzi huo wa Novemba
27 kimakusudi ili aendelee kusalia mamlakani.
Chanzo BBC.
No comments