Rais Magufuli akerwa na Polisi Jamii
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli
amekataa uwepo wa Polisi Jamii nchini na kusema Polisi kushirikiana na raia
ndio chanzo cha kuongezeka kwa uhalifu na matukio ya ujambazi.
Rais Magufuli amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam, wakati wa Hafla ya kula
kiapo cha maadili kwa watumishi wa umma ambapo leo Makamishna wa jeshi
la Polisi walioteuliwa hivi karibuni walikuwa wanatekeleza zoezi hilo Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa alipinga uwepo wa Polisi jamii tangu akiwa waziri
wa Uvuvi na kusema kwa sasa ni lazima ifike mahala raia atakapokutana na
polisi amuogope kwa kuwa dunia ya sasa imebadilika na raia abaki kuwa raia
na Polisi abaki na nafasi yake.
Amiri Jeshi Mkuu amewataka Polisi kuchukua hatua za kisheria kukabiliana na
watu wanaovamia vituo vya Polisi ambao wanahatarisha maisha yao na sio
kudai ni Polisi jamii wakati wanavunja sheria.
Lakini Mhe Rais amesisitiza polisi hao wanavyochukua hatua dhidi ya wahalifu
hao wazingatie sheria ili wasionee watu wema ambao wanafata sheria za nchi
kama katiba ya nchi inavyosema.
Aidha amewaahidi kulinda maslahi ya jeshi hilo na kuwawekea mazingira mazuri
ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwaongeza mishahara pamoja na
kuwapandisha vyeo kwa wale ambao wataonekana kufanya vizuri zaidi.

kuwapandisha vyeo kwa wale ambao wataonekana kufanya vizuri zaidi

No comments