Aliyepiga picha mauaji ya Mwangosi afariki
Tasnia ya habari imepata pigo baada ya mpiga picha wa gazeti la Tanzania
Daima aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi, JOSEPH
SENGA,amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini India.
Senga amefariki siku ambayo muuaji wa Daudi Mwangosi amehukumiwa
kifungo cha miaka 15.
Ni yeye aliyepiga picha iliyochapishwa sana kwenye magazeti na mitandao ya
kijamii ikionyesha jinsi Mwangosi alivyouawa.
Licha ya kukabiliwa na mazingira magumu siku hiyo, Senga,anabaki kuwa
shujaa kwa kuhatarisha maisha yake.
Alisimama bila woga,akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi
wenye silaha,huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,
milio ya risasi ikisikika,na kuzitunza, zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi.
Pengine bila yeye leo hii yawezekana kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu
dhidi ya aliyemuua Mwangosi ingekuwa ndoto.
Senga amefariki nchini India alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu ya
ugonjwa wa Moyo.
Mungu ailaze roho yake mahali pema, AMEN.

No comments