Koffi afungwa jela
Mwanamuziki mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Koffi
Olomide amehukumiwa kifungo cha miezi 18 na Mahakama moja Kinshasa,
DRC.
Koffi alikamatwa mapema leo nyumbani kwake Kinshasa na kufikishwa
Mahakamani akituhumiwa kufanya shambulizi la mwili kwa mmoja wa
wanenguaji wake.
Ijumaa iliyopita akiwa kwenye uwanja wa ndage wa Jomo Kenyatta nchini
Kenya, Koffi alidaiwa kufanya shambulizi hilo.
Kipande cha video kilichosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku hiyo
kilimuonyesha Koffi akimpiga teke mnenguaji wake aliyekuwa anaonekana
kubishana na mnenguaji mwingine wa bendi hiyo ambaye anadaiwa kuwa na
uhusiano wa Kimapnzi na Koffi tangu mwaka 2012.
Tukio hilo lilimfanya Koffi atimuliwe nchini Kenya hivyo kushindwa kufanya
tamasha lililokuwa limepangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.
Aidha nyumbani kwao DRC, watetezi wa haki za binadamu walianzisha kampeni
kuishinikiza Serikali imkamate Koffi kisha afikishwe Mahakamani kuadhibiwa
kutokana na tukio hilo la aibu alilofanya.
Ndipo leo alipokamatwa nyumbani kwake, akafikishwa Mahakamani, akakiri
kutenda kosa hilo na kuhukumiwa jela miezi 18 adhabu ambayo atalazimika
kutumikia mwaka mmoja jela.

No comments