Rais Magufuli aibua ufisadi mwingine wa mabilioni ya shilingi ndani ya Jeshi la Polisi

Rais Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na vitendo vya rushwa
ambavyo vilinafanya jeshi hilo kukosa heshima katika jamii huku akisema kuwa
ana taarifa za jeshi hilo kuingia katika makubaliano ya kifisadi ya mabilioni ya
shilingi kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha makamishna wa
Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisha
kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini hadi leo hakuna hata
sare moja ya iliyonuuliwa.

Ameshangazwa na jeshi hilo kutoa kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa kati ya
shilingi bilioni 40 hadi 60 kwa ajili ya sare za polisi ambazo hadi leo hakuna
hata moja iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi hilo likikosa shilingi bilioni 4 tu
za kukomboa magari yao zaidi ya 70 yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) huko bandarini.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe
mbele ya haki ila angalau hata nusu ya fedha hizo ziweze kurudishwa zikalipie
magari ya polisi yaweze kutoka bandarini maramoja.

Amelitaka pia Jeshi la Polisi kuachana na utaratibu wa kuwa na watumishi
ambao ni raia wa kawaida na badala yake polisi wenyewe ndio washike nafasi
hizo kulingana na taaluma husika na kushangazwa na taarifa kuwa Mhasibu
Mkuu wa Polisi aliyetumbuliwa hivi karibuni kwa tuhuma za ubadhirifu alikuwa
raia wa kawaida na sio polisi.

No comments