POSSI: JAMII IWASHIRIKISHE WATU WENYE ULEMAVU KATIKA FURSA ZOTE ZA MAENDELEO
Na.Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu,
Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameiasa jamii
kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli zote za maendeleo ili
kusaidia kuwainua na kuondokana na dhana ya utegemezi na kuwakwamua kiuchumi.
Dkt.Possi
ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Wilaya za Mbinga, Songea
Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma ambapo alitembelea Shule
zenye kuhudumia watu wenye
mahitaji maalum za Songea Boys, Luhira, Huruma na Kituo cha Kulelea wenye
ulewavu cha Peramiho
Disabled Persons Action (PEDIPA) na
Kituo cha kulele wazee na wenye ukoma cha Nge Wilayani Nyasa.
Katika
ziara hiyo Mhe.Possi alibaini changamoto nyingi za watu wenye
ulemavu na kuishauri jamii namna pekee ya kutatua changamoto wanazokabiliana
nazo ni jamii kuona umuhimu wa kuwashirikisha watu hao katika mipango yote ya
maendeleo.
“Halmashauri
ziandae mipango ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kushiriki kikamilifu
katika kujitafutia kipato na hii itasaidia kuondokana na hali ya utegemezi na
kuondoa mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwa hawawezi” .Alisema
Mhe.Possi.
Waziri Possi alisisitiza kuwa ni lazima Halmashauri ziwe na
ubunifu wa miradi ya maendeleo itakayo walenga watu wenye ulemavu, “Ni vyema
sasa kuwe na jitihada za makusudi za kuunda miradi maalum kwa ajili ya kuwapa
nafasi za ushiriki ili kujitafutia vipato na kuyakabili mazingira yao,
ikumbukwe wakina mama waliachwa nyuma kwa muda mrefu ila baada ya kupaza sauti
zao tunaona sasa wanasikika hivyo hivyo iwe kwa watu wenye ulemavu” Alisitiza
Dkt.Possi.
Aidha
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Dkt.Osca Albano alisisitiza kuyapokea
maelekezo yote ya Naibu Waziri Mhe.Possi kwa vitendo na kumhakikishia kuwa
Wilaya yao itakuwa mstari wa mbele katika kulitekeleza hilo.
“Sisi
tunafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Halmashauri hivyo ni vyema tukalichukua
hilo kuangalia namna tunavyoweza kuliweka katika mipango yetu yote ya maendeleo
ili kuwasaidia na kufikia lengo la serikali,” alisema Dkt. Albano.
Nae Katibu
Tawala Wilaya ya Songea Bw. Edmund Siame aliomba halmashauri zote ziwe zinatoa
mrejesho mapema juu ya maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu huku Mwalimu
Elswida Charles anayehudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum akimweleza Dkt.
Possi kuwa watu wenye ulemavu wanafarijika kutokana na jitihada anazofanya
kuwainua watu wenye ulemavu.



No comments