ANNA MAKINDA ATAKA MABADILIKO YA SHERIA YA NDOA
Spika
mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, ameeleza kusikitishwa na kitendo cha
serikali kushindwa kufanyia marekebisho baadhi ya vifungu vilivyopo
katika sheria ya ndoa ya mwaka 71 licha ya mchakato kuanza muda mrefu
hali inayosababisha vitendo vya ukatili kuendelea.
Makinda
ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, kwenye kongamano la kwanza
kitaifa kutetea na kusimamia haki za wanawake kwa kuwawezesha na
kusimamia kiuchumi ambapo amesema baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye
sheria ya ndoa inayotumika sasa vinakiuka na kukandamiza haki za
wanawake hasa wale wasio na uelewa wa kisheria.
“Ningeomba
serikali isaidie kufinance kucontribute kwasababu development partners
kweli wanatusaidia watafika siku nyingine wataondoka. Tumemaliza si
wanawapaga muda mradi wa miaka miwili mitatu subject to renew au basi
kabisa, wanakuja viongozi wa nchi yanakuwa majitu wanasema hayo mambo
out tutaweza kweli,” alisema.
“Sheria
ya ndoa ya mwaka 71 inachelewa wapi? Tumeiimba wee toka mi nikiwa
waziri mpaka leo kuna tatizo gani ile si iliandikwa na watu tu?,”
alihoji.
No comments