AJALI ZA VIFO ZAPUNGUA KWA ASILIMIA ISHIRINI NA NNE
Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha (SSP) Nuru
Kacharia akitoa takwimu juu ya hali ya usalama barabarani kwa wananchi
wa Arusha wakati wa uzinduzi ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani
iliyofanyika jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
|
| Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles kumbo akitoa shukrani kwa wadau wa kampuni mbalimbali wakiwemo na waandishi wa habari katika kufanikisha sherehe za wiki ya nenda kwa usalama barabarani. |
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro (aliyekaa katikati
mwenye suti) ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa kwenye uzinduzi ya wiki
ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Arusha akiwa katika picha ya
pamoja na wadau mbalimbali.
|
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Koplo Athilio Choga
akimuelezea mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro
(Mwenye suti) namna ya mpangalio wa mji unavyoweza kupanua barabara ili
kuepukana na ajali.

Katika kipindi cha toka Januari mpaka Oktoba mwaka 2016 ajali za vifo zimepungua kwa asilimia ishirini na nne ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2015, ambapo kulikuwa na jumla ya ajali za vifo 74 tofauti na mwaka huu kumekuwa na ajali 56 ambapo ni sawa na upungufu ya ajali 18 ambazo ni 24% .
Picha
no. 5. Askari wa Brass Bendi ya Polisi toka Chuo cha Polisi Moshi
wakiwa wanatoa heshima jukwaani wakati wakipita mbele ya mgeni rasmi Mh.
Gabriel Daqarro mkuu wa wilaya ya Arusha wakati wa uzinduzi ya wiki ya
Nenda kwa usalama Barabarani mkoani hapa.
ARUSHA
ARUSHA
Katika kipindi cha toka Januari mpaka Oktoba mwaka 2016 ajali za vifo zimepungua kwa asilimia ishirini na nne ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2015, ambapo kulikuwa na jumla ya ajali za vifo 74 tofauti na mwaka huu kumekuwa na ajali 56 ambapo ni sawa na upungufu ya ajali 18 ambazo ni 24% .
Akitoa takwimu hizo katika sherehe za uzinduzi ya wiki ya
nenda kwa Usalama Barabarani zilizofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mkuu
wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoani hapa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP)
Nuru Kacharia alisema kwamba katika ajali hizo 74 kwa mwaka 2015 jumla ya watu
97 walipoteza maisha na mwaka huu 2016 kwa kipindi kama hicho ajali hizo ni 56 ambazo
zilisababisha vifo vya watu 68.
Kacharia aliendelea kubainisha kwamba, mbali na upungufu wa
ajali za vifo lakini kikosi hicho cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali wameweza pia kupunguza ajali za majeruhi kwa 5% ambapo mwaka
2015 kuanzia Januari hadi Oktoba ajali zilizosababisha majeruhi zilikuwa 763 tofauti
na ajali zilizosababisha majeruhi 725 kwa kipindi kama hicho kwa mwaka huu wa
2016.
“Asilimia 75 ya ajalli za barabarani zinasababishwa na
wanadamu kwa kutotii sheria za barabarani, madereva kuendesha vyombo vya
usafiri wakiwa walevi, kuendesha kwa mwendokasi, watembea kwa miguu na waenda
mikokoteni kutofuata sheria”. Alifafanua Mkuu huyo wa Usalama Barabarani.
Alisema mbali na makosa ya kibinadamu lakini pia, ubovu wa
vyombo vya usafiri kama vile uchakavu wa magurudumu na kadhalika husababisha
ajali kwa asilimia kumi na tano pamoja namiundo mbinu ya barabarainachangia kwa
asilimia kumi.
Alisema kwamba kwa mwaka huu wa 2016 Kikosi cha Usalama
Barabarani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa vyuo vya udereva wameweza
kutoa elimu kwa jumla ya wadereva 73,830 wa vyombo vya usafiri, huku vituo
2,149 vya pikipiki wanachama wake walipata elimu sahihi ya matumizi ya
barabarani, na kuongeza kwamba jumla ya vipindi 624 vya redio sawa na dakika
18,720 zilitumika katika kuwaelimisha watumiaji wa barabara kwa mwaka huu wa 2016.
Akizindua rasmi wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani mkoani
hapa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mara baada ya ukaguzi wa vibanda
mbalimbali vilivyomo ndani ya uwanja huo, Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro
alisema kwamba ajali za barabarani zimeendelea kugharimu maisha ya watu wengi
hivyo kuathiri ustawi wa jamii pamoja na uchumi kwa ujumla.
Alisema kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua ili
kupunguza ajali na kuiagiza kamati na taasisi husika kuweka mikakati madhubuti
kama vile kupendekeza marekebisho ya sheri za usalama barabarani, wakala wa
barabara waweke alama za barabarani ili zitoe uelewa sahihi kwa watumiaji wa
barabara na kuliomba Jeshi la Polisi washirikiane na wadau wengine liweze kutoa
mafunzo ya mara kwa mara hasa kwa waendesha pikipiki ili ajali hizo ziweze
kupungua.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu
Kamishna (DCP) Charles Mkumbo ambaye pia ni mlezi wa Kamati ya Usalama
Barabarani alisema kwamba, kamati hiyo itatekeleza yote yaliyoagizwa na Mkuu wa
Mkoa na kuwashukuru wadau wote pamoja na vyombo mbalimbali vya habari kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani na kuahidi
kuongeza jitihada za kila aina ili kuweza kupunguza ajali .
Katika sherehe hizo za uzinduzi zilizokuwa na kauli mbiu “Hatutaki ajali tunataka kuishi salama”
Jeshi la Polisi liliwatunuku vyeti wadau mbalimbali pamoja na Mtangazaji wa
kituo cha Televisheni cha Star TV mkoani
hapa Ramadhani Mvungi na Radio Triple “A” kwa kutoa mchango mkubwa katika
uelimishaji wa jamii juu ya Usalama Barabarani mkoani hapa.
No comments