Kwa Picha: Moto mkubwa watishia Israel
|
Misitu iliyo karibu na
Jerusalem pia inatishiwa. Israel imepokea usaidizi kutoka Urusi,
Uturuki, Ugiriki, Italia, Croatia na Cyprus.
|
| Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makwao baada ya moto mkubwa
kuendelea kuenea na kukaribia kufika katika mji wa Haifa, kaskazini mwa
nchi hiyo. |
|
Moshi kutoka kwa moto huo Haifa wakati mwingine ulikuwa mwingi kiasi kwamba karibu jua lizibwe.
|
AFP
Misitu iliyo karibu na
Jerusalem pia inatishiwa. Israel imepokea usaidizi kutoka Urusi,
Uturuki, Ugiriki, Italia, Croatia na Cyprus
|
|
Hakujaripotiwa taarifa zozote
za watu kuumia vibaya lakini watu kadha wamepelekwa hospitalini
wakikabiliwa na matatizo kutokana na kupumua hewa iliyojaa moshi.
|
|
EPA
Ukosefu wa unyevu kwenye hewa pamoja na kuwepo kwa upepo mkali kumesababisha moto huo kuenea upesi.
|
|
Maelfu ya wakazi wamehama makwao Haifa, wakijaribu kunusuru mali yao.
|
|
Moto huo hapa unaonekana ukiwaka karibu na barabara kuu ya Route 1 inayounganisha Tel Aviv na Jerusalem.
|
|
Wazimamoto wanaendelea na
juhudi za kukabiliana na moto huo, ingawa umeathiri maeneo makubwa na
wazimamoto hao ni wachache. Wanahitajika pia kuwalinda raia na nyumba
zisishike moto.
|
No comments