Uzinduzi wa Mjengoni Club Arusha mambo yalikuwa hivi :tazama picha mbalimbali hapa
Mkurugenzi wa
mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John Mdeme akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa uzinduzi huo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kiongozi wa bendi ya Mjengoni Classic Robert Mukongya (Digital) akifafanuajambo mbele ya waandishi wa habari waliouthuria uzinduzi huo.picha naVero Ignatus blog.
Mjengoni
classic Band ikiwa inatumbuiza siku yauzinduzi wa mjengoni club,siku
hiyo walizindua pia vyombo vyao vipya.Picha na Vero Ignatus Blog. 

Sheif
akifanyayake siku hiyo ya uzinduzi wa mjengoni club hapa wanaonekana
wateja wakiagiza nyama choma ya kuku kama inavyoonekana pichani.picha
na Vero Ignatus Blog.
Mashabiki
na wapenzi wa bendi ya mjengoni wakiwa wanasakata rumba hatariii
.,Palikuwa hapatoshi ni mwendo wa kutoka jasho wakati kunabaridi.
Msaniii wa bendi ya Fm Academia Kingombe Blaise na aliuthuria katika uzinduzi huu wa bandi ya mjengoni pamoja na klabu mpya matata ya Mjengoni
Hapa wanahabari hawakucheza mbali,Mmiliki
wa blog ya libenee la kaskazini Woinde Shizza wa kwanza kulia nyuma
yake ni mmiliki wa blog ya Jamii blog Pamela mollel ,wakanza kushoto
ni dada Fatuma wa Stax Tv pamoja na Mmiliki wa Veronica Ignatus Blog wote tulibahatika
kuhuthuria na kushuhudia uzinduzi rasmi wa bendi ya mjengoni pamoja na
klabu ya mjengoni
Burudani ikiendelea kutoka kwa bendi ya mjengoni
Mmiliki wa jamii blog Pamela mollel akiwa anafafanua jambo kuhusiana na kiota iki kipya kilichozinduliwa rasmi jijini Arusha ambapo alitumia muda huo kuwa sihi wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na wale wageni ambao wanauthuria katika mkoa huu kutoacha kufika mjengoni klabu kwa ajili ya kujipatia nyama choma safi na freshi pamoja na muziki muzuri kutoka katiak bendi ya mjengoni club.
Na. Vero Ignatus Arusha
Club
ya ijulikanayo kwa jina la Mjengoni Club imezinduliwa hivi karibuni
jijini Arusha,wakati huo huo ukafanyika uzinduziwa MjengoniClassic
Bandi pamoja na uzinduzi wa vyombo vipya vya bendi hiyo.
Akiongea
na waandishi wa habari
katika usiku wa uzinduzi rasmi wa Club hiyo hiyo mkurugenzi mtendaji wa
John Mdenye amesema kuwa wakazi wa Arusha muda mrefu wamekuwa na kiu ya
kuwa na bendi , ambayo wanaweza kukaa na kujiburudisha wakati wa
wikiendi,waeamua kufanya hiyo kwaajili ya wakazi wa Arusha pamoja na
mikoa jirani.
"unajua
tangia kufungwa kwa ukumbi wa sabasaba haijawahi kubendi nzuri amabayo
ina vyombo vizuri na wapigaji wazuri lakini sisi hapa mjengoni Club
mtaiona hii mjengoni classic band kwakweli wakazi wa Arusha wataifurahia
sana"alisema John.
Mkurugenzi huyo mtendaji wa
mjengoni Klabu pamoja na mjengoni Bendi John mdeme mesema kuwa ameamua kufungua kiota ichikipya
ili wakazi wa jiji la arusha wawez e kupata sehemu ya kistaarabu ya kupata
chakula ,nyama choma nzuri pamoja na mziki mzuri wa mubashara bandi
Kwa upande wakekiongozi wa Mjengoni Classic Band Robert Mukongya (Digital) amesema kuwa
wamejipanga kufanya mkoa wa Arusha kuwa na bendi kubwa inayotoa burudani ya
nguvu kama zilivyo bandi zingine za jiji la Dar es salaam akatolea mfano FM
Academia na malaika bendi.
Digital amesema kuwa wakazi wa mikoani wamekuwa
wakitegemea bendi kutoka jijini Dar-es-salaam lakini kwa sasa hivi wamesogezewa burudani karibu kabisa na
itakuwa kila siku za wikiendi ambapo
bendi hiyo inawanamziki wengi ambao wanauwezo wa hali ya juu pamoja na
uzoefu wakutosha amewataka wapenzi wa mziki wa dansi wataipenda bendi
hiyo na kuikubali
"Hadi sasa bendi inazo nyimbo zake na wanajipanga kwa ajili ya kurekodi ili wapenzi ,wadau na wananchi waweze kupata mziki na kuhusikia katika maredio na hata wanapokuwa majumbani kwakusema bendi hiyo ya mjengoni itakuwa inatoa burudani kila wekendi hivyo wakazi wa jiji la Arusha pamoja na mikoa ya jirani na wageni mbalimbali watakaotembelea jijini hapa."alisema Robert.
















No comments