Mahakama yakubali kupokea ripoti ya kichunguzi ya kesi ya Exim benki
| . | Shahidi wa 23 katika kesi ya wizi,kugushi na kutakatisha fedha zaidi ya
shilingi bilioni 7 inayowakabili waliokuwa wafanyakazi 13 wa benki ya Exim
benki tawi la Arusha ,Mratibu Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la polisi Makao Makuu,Crisantus
Kitandala{44} jana alikabidhi ripoti ya kiuchunguzi ya kimaandishi na vielelezo
vyake juu ya wizi uliofanyika katika benki hiyo.
Kitandala ambaye ni Mkuu wa kitengo
cha Maabara ya uchunguzi wa Kisanyansi wa Maandishi ambaye amefanya kazi hiyo
kwa zaidi ya miaka 10 alisema kuwa ripoti hiyo imechunguzwa kwa kutumia mashine
ya kisasa ya video ya Comparator 6000 vsc 6000 na vifaa mbalimbali vyenye uwezo
wa kutambua miandiko mbalimbali inayobishaniwa.
Shahidi huyo alisema hayo wakati
akiongozwa na Mwanasheria wa serikali Mwandamizi ,Poul Kaduchi mbele ya Hakimu
Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Arusha,Deusdedict Kamugisha.
Mtaalamu huyo wa maandishi wa Jeshi
la Polisi alisema kuwa ofisi yake ilipokea vielelezo vilivyokuwa vikibishaniwa vya
benki nya Exim kutoka ofisini ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai{RCO}
Arusha novemba 24 mwaka huu.
Shahidi huyo alisema katika
uchunguzi wake wa unyambulishaji wa kitaalamu na kisayansi wa miandiko katika
vitu vinavyobishaniwa vya nyaraka za kibenki na miandiko ya baadhi ya
watuhumiwa ilibainika baadhi ya miandiko ilikuwa ikifanana na miandiko ya
watuhumiwa wa kesi hiyo.
Alisema bahasha ya vielelezo vya
benki ya Exim ilivyokuwa na mihuri,risiti za kuweka na kutoa ,regista ya
kuingia na kutoka kazini,hundi za kuweka na kutoa na zenye saini ya baadhi ya
watuhumiwa ,fomu mbali za kibenki zilizosainiwa na baadhi ya watuhumiwa
zilikuwa zikifanana na ripoti yake bila ya kuwa na shaka yoyote katika
uchunguzi wake.
Mtaalamu huyo alisema RCO Arusha
alikuwa akitaka uchunguzi ufanyike kulinganisha saini na maandishi na alama za
mihuri zilizokuwa zikibishaniwa na aligunduwa kuwa baadhi ya saini na miandiko
ilikuwa sahihi kwakwa baadhi ya watuhumiwa.
Shahidi aliwataja baadhi ya
watuhumiwa kuwa ni pamoja na Mosses Chacha,Liliani Mgeye,Tutufye Mwakipesile
,Neema Kinabo ,Pamphir Lubuva ,Deusdedict Chacha na Shijana Matumbo na wengine
miandiko yao ilikuwa ikifanana na uchunguzi aliofanya.
‘’Uchunguzi wangu ulikamilika
januari 27 mwaka huu na ripoti ya uchunguzi huo niliipeleka ofisi ya RCO Arusha
siku hiyo hiyo na nakala ya uchunguzi alikabidhiwa Kamishina kwa niaba ya
Mkurugenzi wa kitengo hicho’’alisema Kitandala
Awali kulizuka malumbano ya kisheria
kati ya mawakili wa watuhumiwa ambao walipinga ripoti hiyo kupokelewa na
mahakama kama ushahidi kwa maelezo kuwa ilikuwa
na kasoro mbalimbali za kisheria na mhusika hakupaswa kuitoa yeye mahakamani
hapo.
Hata hivyo Hakimu Kamugisha
alitupilia mbali pingamizi hilo na kumwamuru shahidi kutoa taarifa hizo
mahakamani hapo kama ushahidi kwani yeye ndiye mhusika mkuu wa ripoti hiyo.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikilizwa
tena leo wakati shahidi huyo akiendelea kutoa ushahidi wake kwa siku ya tatu
mfululizo katika mahakama hiyo.
Watuhumiwa katika kesi hiyo ni
pamoja na aliyekuwa meneja wa benki tawi la Exim Arusha Bimel
Gondalia{37},Lilian Mgaya{33} mshitakiwa wa tatu Neema Kinabo{30}ameachiwa
baada ya kukiri kosa na kulipa fainina mshitakiwa na nne ni Livistone
Julius{36}.
Wengine ni pamoja na mshitakiwa wa
tano Joyce Kimaro{36},mshitakiwa wa sita ni Daud Mosha,mshitakiwa wa saba ni
Doroth Tigana{50} Evans Kashebo{40},mshitakiwa na tisa Mosses
Chacha{37}ameachiwa baada ya kukiri kosa na kulipa faini ya shilingi milioni
100 mshitakiwa wa kumi katika kesi hiyo Tuntufe Agrey{32}.
Mshitakiwa wa kumi na moja katika
kesi hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya watu wa Jiji la Arusha ni Joseph
Meck{34},Janes Massawe{32} mshitakiwa wa kumi na mbili,mshitakiwa wa kumi na
tatu ni Christopher Lyimo{34}na mfanyabishara wa Arusha Gervas Hugo ambaye ni
mshitakiwa wa kumi na nne.
Washitakiwa wanne tu ambao ni Gomes
mshitakiwa wa kwanza,mshitakiwa wa nane Kashebo,mshitakiwa wa kumi na moja Meck
na Lyimo wako nje kwa dhamana kwani hawakushitakiwa na shitaka la utakatishaji fedha
lakini washitakiwa wengine wote wako rumande kwa makosa ya utakatishaji
fedha haramu kwani kesi hiyo haina dhamana kwa mujibu wa sheria.
|
No comments