UN: IS wanatekeleza mauaji zaidi kwa wa Iraq
Siku ya jumamosi waliokuwa wafanyakazi wa vikosi vya serikali waliuawa.
Msemaji wa idara ya haki za binadamu wa umoja wa mataifa Kwa mjibu wa umoja wa mataifa, Ravina Shadasani anasema kuwa IS wanadaiwa kuwatumia raia kama ngao yao katika eneo la mapigano, ambapo wamejaribu kuwahamisha raia wapatao 25,000 kutoka mji jirani na Masul na kuwafanya ngome yao.
Kutokana na mbinu hizo za IS, UN Imetoa angalizo kwa vikosi vya serikali ya Iraq kuwa makini wanapo walenga wapiganaji hao, ili kutosababisha madhara kwa raia wa kawaida.
Vikosi vya serikali ya Iraq, kwa sasa vinaendeleza jitihada za kuukomboa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa IS.
No comments