Wachezaji wa Argentina wasikitishwa na habari zinazomhusu Lavezzi kutumia bangi


timu-ya-taifa-ya-argentinaKufuatia chombo kimoja cha habari cha Argentina kuripoti kuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Ezequiel Lavezzi ametolewa katika orodha ya wachezaji ambao watacheza mchezo wa Argentina na Colombia sababu ya kuvuta bangi akiwa kambini, wachezaji wa Argentina wamejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuzungumzia jambo hilo.

Taarifa hizo pia zilisambazwa katika mtandao wa kijamii wa Twitterr na mtangazaji wa Radio Mitre ya Argentina, Gabriel Anello na kuandika “Lavezzi ametolewa katika orodha ya wachezaji wa akiba wa mchezo wa kesho kwa sababu ya kuvuta jana usiku akiwa kambini? Nauliza … nauliza tu”

Wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa hizo, wachezaji wa Argentina wakiongozwa na nahodha wa timu hiyo, Lionel Messi wamesema kuwa wamesikitishwa na taarifa hizo na wameamua kuungana kwa pamoja kupinga taarifa hiyo.

“Tumefanya maamuzi ya kutokuzungumza na vyombo vya habari, ni dhahiri mnafahamu kwanini, kuna shutuma nyingi, kuna mambo mengi ya kuvunja heshima, na shutuma nyingi ni kuhusu `Pocho` (Lavezzi),
“Tunafahamu kuwa wengi wenu hamfanyi hivi vitendo vya kuvunja heshima, tunaweza kukosolewa kama tumefungwa, au tumeshinda au tukiwa tumecheza vizuri au vibaya, lakini hili linahusu maisha ya mtu binafsi, kama hatutaweza kulizua sasa, hatutaweza kulizuia kamwe,” alisema Messi


No comments