Matokea ya mtihani wa darasa la saba kwa Mkoa wa Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema mkoa huo umeshika nafasi ya 8 kati ya mikoa kati ya 26 katika matokeo ya mtihani nwa darasa la saba kwa mwaka 2016 ukilinganisha na mwaka 2015ukilinganisha mkoa ulishika nafasi ya 6 kitaifa.

Akitoa taarifa hiyo katibu tawala wa mkoa Richard  Kwitega amesema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeshuka kwa asilimia 2.09 ambapo ni asilimia 77.58ya ufaulu wote wa mwaka 2016 ukilinganisha na ule wa mwaka 2015 ulikuwa ni asilimia 79.67.

Kwitega amesema mkoa ulisajiliwa wanafunzi 34, 987 ambapo wavulana walikuwa 16,538 na wasicha18,449 waliofanya mtihani wa kuhitimu waliku wa wanafunzi 34,782 ikiwa wavulana 16,538,wasichana 18,360 na wenye mahitaji maalumu wakiwa 46.

Waliofaulu kwa kupata alama za 100-250walikuwa 26,984ikiwa ni wavulana 12,583 na wasichana 14,401 sawa na asilimia sawa na asilimia 77.58 lengo la ufaulu kitaifa kwa mujibu wa Big Result Now ni asilimia 80.

Wilaya ya Monduli ndiyo wilaya pekee mkoani Arusha iliyoweza kuongeza ufaulu kwa asilimia 70% kwa mwaka 2016.

VIWANGO VYA UFAULU KATIKA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA ARUSHA KAMA IFUATAVYO:

1. Halmashauri ya wilaya Jiji 92%nafasi ya ufaulu kitaifa 3
2.Halmashauri ya Arusha 80%
3.Halmashauri ya wilaya ya Karatu   65.49% nafasi ya ufaulu kitaifa     120
4.Halmashauri ya wilaya ya Longido  56 %    nafasi ya ufaulu kitaifa     159
5.Halmashauri ya Wilaya ya Meru      65 .3 %nafasi ya ufaulu kitaifa     119
6.Halmashauri ya wilaya ya Monduli  71%    nafasi ya ufaulu kitaifa        87
7.Halmashauri ya Ngorongoro           67%       nafasi ya ufaulu kitaifa    108  


  



No comments