Mashahidi 3 kutoa ushahidi dhidi ya mwenyekiti UVCCM mkoa Arusha aliyejifanya Afisa usalama wa Taifa
Na.Vero Ignatus ,Arusha
.
Mashahidi wa watatu, akiwepo afisa usalama wa Taifa, mwandamizi,
Editha Aveline watatoa ushahidi katika kesi ya kujifanya usalama wa
taifa inayomkabili, Mwenyekiti wa Umoja wa
Vijana wa CCM(UVCCM) mkoa wa Arusha ,Lengai ole Sabaya.
Wakili wa Serikali Riziki Mahanyu ,alitoa taarifa hiyo jana,Mbele ya hakimu mkazi Gwantwa Mwankuga
wakati akisoma maelezo ya awali ya kesi ya kujifanya afisa usalama
kiongozi huyo wa UVCCM ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sambasha.
Mahayu alisema mashahidi wengine katika kesi hiyo, watakuwa ni lnspekta Rogat pamoja na Meneja wa hoteli Philipo John.
Mahayu alisema mashahidi wengine katika kesi hiyo, watakuwa ni lnspekta Rogat pamoja na Meneja wa hoteli Philipo John.
Alisema Jamhuri pia itawasilisha Kitambulisho cha kugushi cha Sabaya,
kinachodaiwa ni cha usalama na mtuhumiwa ,risiti ya hoteli ya Sky way yenye namba
0983 na hati ya kuchukua mali polisi
Alisema Sabaya ( 29 ) alitenda
makosa hayo Mei 18 mwaka huu, hoteli ya Sky way ,ambako alikaa kwa siku
5 hotelini hapo kwenye vyumba vyenye gharama ya shilingi 30,000 za
kitanzania ,ambako baada ya kuingia hotelini hapo alikabidhi kwa
uongozi wa hoteli simu yake aina ya Samsung pamoja na kitambulisho
hicho
Pia alisema licha ya kukaa siku hizo
,aliondoka bila kutoa taarifa wala kulipa deni la shilingi 309,000
alizokuwa anadaiwa hotelini hapo ,ambako 150,000 ilikuwa ni ya malazi na
159,000 ilikuwa ya vinywaji ,baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kulipa
meneja wa hoteli hiyo ,alipeleka malalamiko hayo kwa balozi na
mwenyekiti wa mtaa na ndipo walipomshauri apeleke kesi hiyo polisi
Aliongeza
baada ya kupeleka kesi hiyo polisi ,alitafutwa na kukamatwa lakini
baada ya kulipa deni alikabidhiwa simu yake na kitambulisho kilikuwa
kipo kituo cha polisi cha kati
Baada ya
kusomewa maelezo ya awali kutoka kwa wakili wa jamhuri ,mwendesha kesi
,hakimu mkazi Mwankuga ,alimuuliza maswali mshtakiwa huyo kuwa
kama jina lake ni sahihi ,kitambulisho ni chake na kama alikamatwa na
polisi
Mshtakiwa Lengai Sabaya ,alikiri
jina ni lake ,na kukiri kuwa kweli alikamatwa na polisi lakini alikana
kuhusishwa na hizo tuhuma ikiwemo kitambulisho hicho .
Kesi hiyo, imepangwa kuanza kusikilizwa Desemba 7 mwaka huu, ambapo kwa mara ya kwanza,Sabaya septemba 19 alisomewa
mashtaka mawili ya kujifanya mtumishi wa umma wa usalama wa taifa pamoja
na kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa taifa chini ya kitengo
cha kikosi maalum
No comments