WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WABUNGE MSIBA WA MHE. TAHIR
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wakiwa wamesimama kimya kwa
dakikika moja kwa heshima ya mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir,
bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Hafidh alifariki dunia usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha
Mbunge wa Dimai Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa
Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma
Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa
Dimani, Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba
11, 2016. Mbunge huyo alifariki dunia mjijini Dodoma usiku wa kuamkia
leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto),
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na
Walemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) na Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas
Kashililah wakisubiri kupokea mwili wa Mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh
Ally Tahir kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma ambako ulisafirishwa kwenda
Zanzibar kwa Mazishi Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Kiongozi wa
Upinzania bungeni, Freeman Mbowe (kulia) wakishuhudia wakati mwili wa
mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir ukipandishwa kwenye ndege katika
uwanja wa ndege wa Dodoma ili kusafirishwe kwenda Zanzibar kwa mazishi
Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.
Bw.
Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa
wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma
kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.
Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa
Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge
wote.“Tumepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika
wakati mgumu sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.
Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu,
tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha
kuondokewa na mpendwa wao.”
Bw.
Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya
Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti
yanamkuta.Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya
michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi
wa timu ya soka ya Bunge.
Hadi
jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi
wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma
ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, NOVEMBA 11, 2016
No comments