MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI ARUHUSIWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIPOKUWA AMELAZWA
Mke wa Rais wa Tanzania John
Magufuli, Janeth, aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili ameruhusiwa kuondoka hospitalini.Taarifa nyingine iliyotolewa na ikulu Ijumaa imesema ameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya afya yake kuimarika na akarejea nyumbani.
Ikulu imesema Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini Jumatano baada ya "kuugua ghafla na kupoteza fahamu".
"Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda
kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara," alisema kabla ya kuondoka hospitalini.
"Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu."
Novemba mwaka jana, siku chache baada ya kuapishwa hospitali hiyo ni miongoni mwa taasisi za serikali ambapo Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza.
Alisema alisikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini.
No comments