Aliyewahi kuwa waziri wa Elimu Tanzania Joseph Mungai amefariki dunia
Waziri wa zamani na Mbunge wa jimbo la Mufundi Kaskazini Mkoani Iringa, Joseph Mungai amefariki dunia jioni ya leo jijini Dar es Salaam.
Aliyewahi kuwa waziri wa Elimu Tanzania Joseph Mungai amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu
Geofrey Mungai mtoto wa Marehemu amesema marehemu alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuanza kutapika mfululizo na kudhaniwa kwamba alikuwa amekula kitu kibaya.
Afisa Uhusiano wa Hospitali wa Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema mwili wa Marehemu Mungai umepokelewa katika idara ya magonjwa ya dharura na kuthibitisha kifo saa 11:20 jioni
Amesema mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alikihama chama chake cha CCM na kujiunga na chama cha siasa cha CHADEMA katika harakati za uchaguzi mkuu mwaka 2015.
No comments