DC Hapi aagiza mratibu wa TASAF Kinondoni kuvuliawa cheo
Kaya 1,397 zisizo na sifa wilayani Kinondoni zimepokea fedha za mradi wa kuwezesha kaya masikini (TASAF).
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally
Hapi amesema kwa mujibu wa uhakiki uliofanywa na TASAF hivi karibuni,
imebainika kuwa kaya 517 ziliorodheshwa katika orodha ya wanaostahili
kupewa fedha za msaada, na kupewa zaidi ya milioni 180 katika awamu
tofauti, hali zao kiuchumi zinaridhisha na kwamba zimeondolewa katika
mradi huo.
Pia, Hapi amesema uhakiki huo
umebaini kuwa kaya 537 zilizopokea fedha za msaada zaidi ya sh. 266
Milioni hazijulikani makazi yake katika wilaya hiyo, wakati kaya 59
zikibainika hazina makazi huku 15 zikichukua fedha hizo zaidi ya mara
moja na 265 zilihama makazi.
Kufuatia ubadhirifu huo wa fedha,
Hapi amemuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
kumvua cheo Mratibu wa TASAF wilayani Kinondoni Onesmo Kweyamba kwa
kushindwa tekeleza majukumu yake na kuruhusu baadhi ya watumishi wa
serikali, wafanyabiashara na kaya zenye uwezo kupata fedha za msaada.
Aidha, ameagiza vyombo vya dola
kwa kushirikiana na TASAF kufanya uhakiki tena na kwamba kata
itakayobainika kuwa imeorodhesha kaya zenye uwezo kwa ajili ya kupewa
fedha hizo, mwenyekiti wake anachukuliwa hatua za kisheria.
Amesema majina ya kaya zisizo na sifa yatabandikwa katika maeneo husika ili zijijue kisha kurudisha fedha zote ilizopokea.
No comments