Rais wa Korea Kusini alinunua dawa za Viagra

Park Geun-hye

Kashfa nchini Korea Kusini inayohusisha maisha ya faragha ya rais Park Geun-hye imechukua mwelekeo usio wa kawaida huku ikidaiwa kuwa ofisi yake ilinunua dawa nyingi za kuongeza nguvu za kiume Viagra .

Msemaji wa serikali amesema kuwa takriban dawa 400 zinazotumiwa kutibu tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume zilinunuliwa kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na tofauti ya hali ya anga Afrika mashariki,ijapokuwa dawa hizo hazikutumika.

Hayo yanajiri huku kukiwa na shutuma kwamba kiongozi huyo wa Korea Kusini aliruhusu urafiki mrefu kushawishi maamuzi yake kuhusu maswala ya kitaifa na kile rais huyo alichovaa.

No comments