Mfanyabiashara Mtanzania mwenye asili ya Asia amamepandishwa kizimbani kwa kuhujumu uchumi kwa njia ya mitandao
Mtanzania mwenye asili ya Asia Firoz Khan,
amepandishwa mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Arusha kujibu mashtaka ya
kuingiza mtambo wa mawasiliano na kufanya utapeli kupitia njia ya
mawasiliano
Awali, Akisomewa mashtaka hayo na wakili wa Serikali
Johovanes Zacharia alisema mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa 7 ya
kufanya udanganyifu wa mitandao uliopelekea kuliingizia taifa hasara ya
600 milioni.
Akitaja makosa hayo alisema ni pamoja na kuingiza mtambo
wa mawasiliano bila kibali,kutengeneza njia ya mawasiliano kwaajili ya
kukwepa tozo za mawasiliano ndani na nje ya nchi, kutumia mtambo huo
kinyume na sheria ya mawasiliano, kufanya udanganyifu wa kujinufaisha
za nje, kujifanya ni wakala wa usajili wa laini za simu bila
kutambulika, kusajili watu wasitambulika
Awali wakili huyo aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo
alitenda makosa hayo mnamo mwezi wa Tatu na aprili mwaka jana na
kuachiwa kwa dhamana kutokana na sababu ambazo zimempa mamlaka
Mkurugenzi wa mashtaka mahakama imemuondolea kesi mbili na kumfungulia
upya tena kesi huku ikiweka pingamizi ya dhamana ya mtuhumiwa huyo
"Mkurugenzi wa mashtaka ametoa hati ya kumnyima dhamana mtuhumiwa na imewasilishwa mahakamani tayari,"alisema Johovanes.
Upande wa wakili wa utetezi wa mtuhumiwa huyo, aliiomba
mahakama impe dhamana mteja wake kutokana na kushtakiwa kwa kosa
linalofanana kama hilo kwa kwa mara pili.
Pia alisema, mteja wake anahaki ya kupwa dhamana kwakua
Mkurugenzi wa makosa ya jinai alishindwa kuonesha sababu zitakazomnyima
dhamana mtuhumiwa huyo
"DPP hajaonesha sababu kuwa ni ni madhara yapi yako kwa mtuhumiwa akiwepa dhamana au itaathiri vip kesi hiyo akiwa nje kwa dhamana.
"Sielewi ni kwanini mtuhumiwa anafunguliwa kesi, inafungwa halafu imefunguliwa tena"alisema wakili wa mshatakiwa.
Kwa upande wake mwanasheria wa mamlaka ya mawasiliani TCRA amesema kuwa mtu yeyote yule atakayetumia mitandao vibaya sheria itachukua mkondo wake.
No comments